Header

Tangazo moja la biashara kwenye ukurasa wa Instagram wa Beyonce hugharimu shilingi bilioni 2.2

Post ya Beyonce kwenye Instagram iliyomuonesha akiwa mjamzito wa watoto mapacha kwa mara ya kwanza, iliweka historia kwakuwa picha iliyopata likes nyingi zaidi kwenye Instagram – milioni 10.9.

Staa huyo ambaye hufanya interview kwa nadra na kutumia mitandao ya kijamii mara chache tu, amejiweka katika mazingira ghali, maana yake ni kuwa anaweza kuingiza mamilioni ya dola kwa post zake tu.

Kwa mujubu wa kampuni ya D’Marie Analytics, Beyonce ndiye mtu anayeuza zaidi kwenye mitandao ya kijamii, maana yake ni kuwa ana thamani ya kutoza dola milioni 1 (zaidi ya shilingi bilioni 2.2) kwa post moja tu.

Kwa sababu Queen Bey huweka endorsement mara chache sana, post zake zina thamani zaidi kuliko staa yeyote ambao huweka post za matangazo kadhaa kwa mwezi. Kwanza, amewahi kuweka matangazo mawili tu ya biashara kwenye Instagram. La kwanza ni endorsement ya Pepsi, mwaka endorsement ambayo ilikuwa na thamani ya paundi milioni 40.

Pia alitangaza filamu ya Fifty Shades of Grey kwa sababu alikuwa na wimbo wake katika soundtrack. Mastaa wengine wenye thamani kubwa ni Selena Gomez mwenye followers milioni 116 na Rihanna.

Comments

comments

You may also like ...