Header

Rekodi ya Mbao FC yawaweka roho juu Wanamsimbazi

Klabu ya Simba leo itakuwa na kibarua kigumu cha kusaka pointi 3 dhidi ya Mbao FC kwenye uwanja wa CCM Kirumba ambao Azam FC na Mtibwa Sugar ziliangukia pua kwa vipigo kutoka kwa timu hio iliyopanda daraja msimu huu.

Wanarambaramba Azam FC walipigwa mabao 2-1 na Mtibwa Sugar iliambulia kipigo cha mbwa mwizi cha mabao 5-0, pia timu ya Ruvu Shooting ilionja joto ya jiwe kwa Mbao kwa kupigwa 3-1.

Kwa matokeo hayo na mengine yanadhihirisha kuwa Mbao FC sio timu ya mchezo mchezokwani hata mechi ya kwanza baina yao,Simba walihitaji kukaza msuli kuondoka na pointi tatu jijini Dar es salaam kwa ushindi mwembamba wa bao 1-0.

DizzimOnline imeongea na baadhi ya Mashabiki wa klabu ya Simba tawi la Kimara wengi wamesema mchezo wa leo utakuwa ni mgumu sana kwani klabu ya Mbao FC ni wagumu wakiwa nyumbani kwao.

Simba wanahitaji ushindi ili kurudi kileleni na kuendelea kuweka hai matumaini ya ubingwa kufuatia kipigo cha mabao 2-1 kutoka kwa Kagera Sugar wiki iliyopita.

Comments

comments

You may also like ...