Header

Roma kujibu maswali yote magumu Mchana wa leo April 10.

Maswali mengi ya Watanzania ni kujua wapi walipokuwa wakina Roma na nini kiliwapata,nini kilitokea baada ya wao kutoweka sehemu isiyojulikana,majibu ya maswali yote hayo yanatolewa mchana wa leo mbele ya waandishi wa habari kwenye ukumbi wa Serikali wa Habari maelezo ulioko Posta.

Roma na wenzie walitoweka kusikojulikana Wiki iliyopita,Jumamosi wakapatikana wakiwa kituo cha Polisi cha Oysterbay ambapo baada ya kufikishwa hapo taratibu za kiusalama zilifuata ikiwa pamoja na kuwapeleka hospitali kwa ajili ya kuchekiwa afya zao,Dizzim Online iko live kutoka ukumbi wa Habari Maelezo kwa ajili ya kukufahamisha kila kinachozungumzwa.

Comments

comments

You may also like ...