Header

50 Cent amtwanga makonde shabiki

Kutoka Marekani ni rapa, muigizaji na mtayarishaji wa muziki muite Curtis James Jackson a.k.a 50 Cent ameshindwa kuvumilia baada ya kuingia katika jukwaa kwa kuanza kusalimiana na mashabiki kabla ya show jambo ambalo hakulitegema lilitokea.

Katika tour ilipewa jina la #FAIBTOUR mjini Baltimore, Maryland usiku wa jumamosi tarehe 8 ya mwezi huu 50 Cent na mwenzake The Lox kwenye show na alipanda jukwaani kabla ya kuanza kuperform alipitisha mkono kwa mashabiki kwa ishara ya salamu ndipo shabiki mmoja wa kike alipomng’ng’ani mkono wake huku akimvuta tukio lilioambata na 50 kumpiga ngumi ya kifua shabiki yule.

50 Cent punches his female fan-Dizzim Online

Picha ya 50 Cent kuvutwa na shabiki

Ndani ya muda wa tukio hilo kutokea rapa mpya aliyesainiwa chini ya G Unit st Uncle Murda kwa kusaidiana wahusika wa usalama waliweka mambo sawa kwa kumrudisha na baada ya 50 Cent kurudi jukwaani aliwataka vijana wa usalama wampandishe shabiki yule jukwaani. Shabiki alionekana kutoumizwa zaidi na kitendo cha 5o kumpiga ngumi bali alipopanda jukwaani alicheza kwa furaha huku rapa Uncle Murda alipokuwa akiperform wimbo wake ‘Rap-Up 2016’.

 

Comments

comments

You may also like ...