Header

‘Muziki wa Bongo Fleva unaelekea kufa’ – Pancho Latino

Mtayarishaji wa muziki wa Bongo Fleva mkali kutoka bongo ambae anafanya kazi zake chini ya Studio za B-Hits Pancho Latino ni moja watu wanaoamini kuwa muziki wetu  wa Tanznia unaelekea kufa .

Pancho amesema muziki wetu unabaki kudumaa kila kukicha kwani wakali wengi wanaosifiwa ni walewale wakongwe hakuna vipaji vipya vinavyonolewa kwenye kiwanda cha Muziki kitu ambacho kitapelekea muziki wetu kukwama siku za usoni.

Producer wa sasa siwezi kuwaongelea sana kwa sababu kila producer anafocus yake kwenye muziki na kwenye career yake plan yake ni kufanya nini na kufaidika nini, Kwa hiyo general muziki wa bongo,unaelekea kufa na hatuna cha kufanya na kwa sababu hiyo inabidi system ibadilike kwa sababu toka miaka sisi tunaanza kusikiliza muziki kabla hatujaanza kufanya na tukafanya muziki ndo ule ule system ndo ile ile hakuna watu wapya ambao wanatengenezwa tuseme everyday wakawa wakubwa, kulikoni malegend wale wa zamani wamebaki kuwa wakubwa ila kuna wasanii wamebaki katikati“Amesema Pancho Latino kwenye mahojiano yake na Dizzim Online.

Aliendelea kwa kusema “Sasa why tusiwafanye wasanii wachanga wawe wakali na kukubali vipaji vipya everyday kulikoni kutengeneza watu ambao tuna hisi ni wakali kumbe sio wakali kwa hiyo nafikiria cha kufanya ni ku’focus kubadili system nzima ya muziki baada ya hapo vitu vitaenda sawa sio kufata trend ya muziki unaovuma duniani producers wawe creative kuleta muziki mzuri

Comments

comments

You may also like ...