Header

Steven Gerrard kurejea ndani ya Liverpool

Nahodha wa zamani wa Klabu ya Liverpool maarufu kama Majogoo ya Jiji Muingireza Steven Gerrard anatalajiwa kurudi klabuni hapo msimu ujao ila akirudi kama kocha.

Sky sport wanaripoti  kwamba Gerrard ambaye kwa sasa ana umri wa miaka 36 anatarajiwa kurudi Liverpool mwakani mwezi Januari ili kukinoa kikosi cha vijana U18 huku ukitizamiwa kuwa inawezakana siku moja akipewa kikosi cha kwanza.

Steven Gerrard amecheza Liverpool na kufanikiwa kushinda mataji yote  kwenye ngazi ya klabu huku akikosa  bahati yakunyakuwa kombe la Ligi Kuu nchi Uingereza kwenye maisha yake ya mpira ndani ya Liverpool.

Comments

comments

You may also like ...