Header

‘Watu wanaweka bando kufuatilia ubuyu..’ – Mwana FA

Msanii wa hip hop kutoka Tanzania Mwana FA ameweka wazi kuwa kundi lao la Zamani la East Coast Team haliwezi kurudi tena kama taarifa za awali zilivyodai kuwa huenda wakarudisha kundi hilo.

Mwana FA amesema kwa sasa wataendelea kushirikiana ila kuhusu kuirudisha East Coast Team hilo haliwezekani na kuhusu kuachia ngoma za Kolabo kati yake na wasanii wenzake kama,AY na GK ni kwamba tayari wamesharekodi na hata yeye ana ngoma nyingi ila anaangalia upepo tuu kuachia ngoma hizo kwani kwa sasa watu wanafuatilia sana ubuyu kwenye mitandao kuliko kazi za wasanii .

Nina muziki mwingi kwenye maktaba wa kutosha nasubiri timing tuu,sasa hivi kuna mambo mengi yanaendelea utatoa wimbo hamna mtu anesikiliza watu wanaweka bando kufuatilia ubuyu tuu,kwahiyo acha patulie kidogo tutaangusha“Alisema Mwana FA kwenye kipindi cha Planet Bongo cha East Africa Radio.

Kuhusu Kolabo yake na Wasanii wenzake wa Zamani wa East Coast Team amesema “Tulifanya ngoma mbili tatu ila hatukukubaliana kuziachia so East Coast haiwezi kurudi kwa pamoja lakini Mimi,GK na AY tunaweza kufanya kazi kwa pamoja kwani ni kitu rahisi

Comments

comments

You may also like ...