Header

Yanga kujifua kwa mara ya mwisho leo

Kikosi cha Yanga kitafanya mazoezi yake ya mwisho jijini Dar es Salaam leo jioni kabla ya kuelekea huko Algeria kwenye mchezo wake wa Marudiano dhidi ya klabu ya MC Alger.
Kwenye mchezo wa Kwanza Klabu ya Yanga iliibuka na ushindi mwembamba wa Goli 1-0,Goli ambalo endapo Yanga watajipanga vizuri basi litawavusha kutinga hatua ya Makundi ya kombe hilo la Shirikisho Barani Afrika kwa kupata sare yoyote ile au kufungwa kwa tofauti ya Goli moja ambalo watalipata ugenini.
Klabu ya Yanga ndiyo wawakilishi pekee wa Tanzania katika michuano ya kimataifa baada ya Azam FC kung’olewa na Mbabane Swallows ya Swaziland.

Comments

comments

You may also like ...