Header

Yanga yadandia Treni kwa mbele!! Yaingilia kati rufaa ya Simba dhidi ya Kagera Sugar

Klabu ya Yanga imeingilia kati kwenye sakata la rufaa ya klabu ya Simba dhidi ya Kagera Sugar iliyolalamia kumchezesha mchezaji Mohamed Fakh mwenye kadi za njano tatu ambazo kisheria hakustahili kucheza kwenye mchezo huo wa ligi kuu.

Yanga leo imetoa tamko lao rasmi kwenda kwa Kamati ya Masaa 24 ya Ligi kuu Tanzania Bara ambayo iliweka kiporo rufaa hiyo wiki iliyopita hadi Alhamisi hii kuwa klabu ya Yanga hawana imani na maamuzi yatakayotolewa juu ya rufaa hiyo kwani kuna fununu kubadilishwa kwa ripoti za mchezo,huku wakidai kuwa kwenye kamati hiyo kuna wanachama Sita waandamizi wa Simba na wawili wa Yanga tu.

Kamati hii imechelea kutoa maamuzi kwa kuandaa ripoti za uongo za michezo dhidi ya Fakhi pia tuna taarifa za kughushiwa email na nyaraka zingine ili kuipa alama tatu Simba SC yenye zaidi ya wajumbe 6 katika kamati hiyo. Kama Yanga tumeanza uchunguzi wetu na kutoa taarifa kwa vyombo husika vya dola pia maamuzi yoyote ya kuibeba Simba tutakwenda mahakamani licha ya sheria za FIFA kukataza hivyo kama hawataki tufike huko lazima haki itendeke,Tumeshavijulisha vyombo husika yaani takukuru na watu wa (cyber crime) na TCRA juu ya uchunguzi wa mawasilano ya waamuzi wote waliosika na kutajwa kwenye rufaa hiyo” Alisema Salumu Mkemi mjumbe kamati kuu ya Yanga SC.

Hata hivyo Ofisi ya Wanajangwani imetoa rai kwa TFF kwa kusema “Ofisi hiyo imetoa rai kwa wakati umefika wa kuundwa kwa kamati zisizo na masilahi pande yoyote ili kuleta haki katika maamuzi mbalimbali ya soka letu. ” Tuache kumtafuta bingwa wa mezani . Sisi tumefungwa karibu mechi tatu na hatujalilia alama za mezani kwanini wao?! Mbona jana wamecheza mchezo mzuri mwishoni na kupata ushindi wa jioni dhidi ya Mbao na hakuna kelele?! tena tunawapongeza kwa come back ile Hiki ndicho mashabiki wa timu hizi wanakitaka Ushindi wa uwanjani sio figisu .

Comments

comments

You may also like ...