Header

Baada ya kichapo cha goli 3-0 dhidi ya Juventus: Andres Iniesta aahidi kugeuza matokeo

Baada ya kichapo cha Goli 3-0 Kiungo mkongwe wa Barcelona, Andres Iniesta amesisitiza kuwa hawajisikii vibaya kwa kipigo hicho kutoka kwa Juventus kulinganisha na hali waliyokuwa nayo baada ya kunyukwa mabao 4-0 na PSG.

Kiungo huyo tegemeo wa Barcelona ametamba kuwa watapindua matokeo hayo katika mechi ya marudiano endapo watarekebisha makosa madogo madogo kwani mchezo wao wa jana amekiri kuwa walipoteana kwenye kipindi cha kwanza.

Hatukuonesha kiwango kizuri hasa kwenye kipindi cha kwanza kwani tuliwaruhusu waingie mara nyingi kwenye eneo la goli letu kitu kilichopelekea kupata magoli mawili mapema ingawaje kipindi cha pili tulirekebisha makosa kidogo,Nadhani tulistahili ushindi ila haikuwa bahati yetu“Alisema Andres Iniesta kwenye mahojiano yake na Mtandao wa Marca.

Barcelona watahitaji kushinda kwa angalau mabao manne kwenye mechi ya marudiano na Juventus,Na Iniesta hana mashaka yoyote anaamini wana uwezo wa kugeuza matokeo nyumbani kwao Nou Camp.

Comments

comments

You may also like ...