Header

Bill Nas achomoa kwa mrembo Nandy

Rapa kutoka Tanzania Bill Nas anayefanya vizuri na kazi yake ya ‘Mazoea’ aliyomshirikisha Mwana FA kufuatia jana kusherehekea  siku ya kufanana kwa siku yake ya kuzaliwa(Birthday) ameleza sababu zinazo fanya waonekane kuwa karibu sana na msanii mrembo anayefanya poa na kazi inayokwenda kwa jina ‘One Day’ Nandy.

Bill Nas aliruka futi kadhaa baada ya kuulizwa kuhusu kuwa kwenye mahusiano na kusema kuwa kilichofanya watu wengi wadhani kuwa kuna kinachoendelea na kusema session za kolabo kadhaa za mara kwa mara ndo zimeleta jambo ambalo amesema sio kweli kwamba wako katika mahusiano.

“hapana Nandy hata sio mshikaji wangu wa karibu hiiivyo, sana sana we having a project kuna wimbo wangu ambao ameshiriki na mimi kuna wimbo wake ambao nimeshiriki kwahiyo zile studio session mbili tatu ni session kama mbili tatu lakini hakuna lingine la ziada zaidi ya ushikaji…unajua ukikaa na mtu ambaye umemzoea kawaida huwezi kuficha vitu hivyo” Alisema Bill Nass alipokuwa akihojiwa kwenye XXL ya Clouds Fm.

Vile vile Nandy alitoa majibu ya hali yake kimahusiano na kusema kuwa yuko single kauli iliyotafsiri kuwa hawako katika mahusiano na Bill Nas ingawaje kumekuwa na uvumi mkubwa sana kuwa anatoka kimahaba na rapa huyo.

Msanii Nandy

“Ahaaaa boyfriend hamna niko single sijapa…Ohooo my God bado niko single” Alisema Nandy alipoulizwa na Lil Ommy kuhusu mahusiano yake hata stori za kuhusu kutoka na Dogo Janja.

Hata hivyo Nandy alimwaga sifa za mwanaume anayemhitaji kimapenzi na nakusema kuwa kutesana ni mambo ya kawaida ila tu kikubwa awe mcha Mungu, muelewa, mvumilivu kwa maana kama ataweza kuvumilia yake naye atakuwa mvumilivu kwake.

 

 

 

 

Comments

comments

You may also like ...