Header

Chelsea na Tottenham wapigana vikumbo kumnasa Alvaro Morata

Mshambuliaji wa Real Madrid na timu ya taifa ya Spain Alvaro Morata ambaye amekuwa hana namba ya kudumu kwenye kikosi cha Zidane ameweka wazi kuwa timu mbili kutoka jiji la London wanaitaji saini yake.

Akizungumza mbele ya wandishi wa habari Morata amesema kuwa mpaka sasa Chelsea na Tottenham zote zina mwitaji na ameshazungumza na makocha wa timu hizo kwa njia ya simu.

Nikweli kuna baadhi ya timu zinaniitaji ila mpaka sasa nimezungumza na kocha Antonio Conte wa Chelsea na mwingine wa Mauricio Pochetttino wa Tottenham Spurs ila ntajua hatima yangu pale msimu utakapoisha.” Alisema Morata

Morata anatazamiwa kuanza leo kwenye mchezo dhidi ya Beyarn Munich kwenye mchezo wa robo fainali ya klabu bingwa Ulaya baada ya kuwa na kiwango kizuri kwenye michezo ya hivi nyuma.

Comments

comments

You may also like ...