Header

Harmonize awajia juu wanaotengeneza matabaka

Msanii wa muziki wa kizazi kipya anayefanya vizuri na ngoma ‘Niambie’ Harmonize ambaye yuko nchini Kenya kikazi(Media Tour) ametoa somo kwa wenye wazo tofauti kuhusu wasanii kufanya muziki wenye maadhi na asili ya tofauti tofauti za nje ya mataifa yao.

Akizungumzia wazo la wengi kulaumu mwenzo huo na kutaka kutenganisha wasanii kufanya muziki wenye asili na miondoko ya nchi nyingine zinazoonekana kukua kimuziki amesema kuwa haoni sababu za kuweka matabaka kwakuwa muziki ni zaidi ya hisia tu na ni vizuri msanii kuwa huru na kufuata kile ambacho kinafanya vizuri kwa kipindi husika ili kusimamisha misingi ya biashara.

“mambo ya kwamba huu ni muziki wa East Africa, huu ni muziki wa West Africa ni ubaguzi. Kwasababu muziki ni biashara wenzetu wanafanyaga tu muziki kwasababu ukizungumzia muziki watu wameanza kuimba hip hop, hip hop asili yake ni marekani unajua mbona watu hawajazungumza…kuchukua muziki wa West Africa kuleta East Africa hivi ni vitu vya kibiashara kwa namna moja ama nyingine lazima tukubali kuwa muziki ni biashara inayobadilika na trending …so muziki inapoingia trending tufanyeni ili tuweze kupata riziki na maisha yetu yazidi kuwa mazuri” Alisema Harminize alipokuwa akihojiwa na AJAABU TV.

Hata hivyo Harmonize amewataka wenye mawazo ya namna hiyo waisome historia ya hip hop na watagundua kuwa imeanzia Marekani na wapo wasanii na wengi hapa barani Afrika wanaofanya muziki wenye chembe za hip hop jambo ambalo amesema kama ingekuwa ni kufuata matabaka hip hop basi sio sawa kufanyika Afrika na mataifa mengine nje ya Marekani.

 

Comments

comments

You may also like ...