Header

Kaburu awatolea uvivu Yanga

Makamu wa Rais wa Klabu ya Simba Geofrey Nyange ‘Kaburu’ amewajia juu Wanajangwani kwa kitendo cha kuingilia kati rufaa yao dhidi ya Kagera Sugar kwa kuwataka waachane na mambo yasiyowahusu.
Kaburu amesema amekuwa akishangazwa na Yanga kuendelea kulivalia njuga suala la Simba kukata rufaa dhidi ya Kagera Sugar kama linawahusu wao kumbe ni suala la Kagera na Simba kusubiria maamuzi ya Kamati ya maamuzi ya saa 72.
Simba imeikatia rufaa Kagera Sugar, Yanga kelele za nini? Hili si suala la nani anasaidiwa na tatizo lipi? Si inajulikana kuwa baada ya kadi tatu za njano nini kinafuatia,Kagera sio Yanga pia kanuni ziko wazi,Hivyo nawashauri waendelee na mambo yao waachane na Simba,“Alisema Kaburu kwenye mahojiano yake na EFM.
Klabu ya Yanga imekuwa ikilalama kuhusiana uamuzi wa Simba kukata rufaa ikipinga Kagera Sugar kumchezesha beki Mohamed Fakhi ikidai alikuwa na kadi tatu za manjano kwenye mechi hiyo iliyochezwa mjini Bukoba wiki iliyopita Simba ilitwangwa kwa mabao 2-1 na wenyeji wake Kagera Sugar.

Comments

comments

You may also like ...