Header

Khloe Kardashian aitamani ndoa na mcheza kikapu mwingine

Mfanyabiashara, mtangazaji na mwanamitindo kutoka katika famiia ya Kardashians ‘Khloe Kardashian’ menye ulevi wa kimapenzi na wanamichezo ashindwa kujizui kwa mcheza kikapu mwingine.

Ndugu huyo mdogo wa kike kwa Kim Kardashian ‘Khloe Kardashian’ aliyeahi kuwa mke wa mcheza kikapu msataafu mmarekanai Lamar Odom amesema kuwa kwasasa anashindwa kuzuia hisia zake za kimapenzi kwa mcheza kikapu maarufu mkanada Tristan Thompson na kuongeza kuwa anatamani waoane ingawaje mcheza kikapu huyo hajamfuata kwa ombi la mahusiano.

Tristan Thompson

 

“ningependa sana niwe na familia,” Khloe aliliambia jarida la ES alipoulizwa kuhusu mahusiano yake na staa wa kikapu wa NBA … “Actually tumeshazungumzia suala hilo” Alimalizia. Alipouliza kuhusu kuletewa maombi ya ndoa Khloe alijibu haraka “Ndio, nitakubali”

 

Jarida la ES ililomhoji Khloe Kardashian

“Najua ni baba tayari, naamini ni mzazi mwema. Na kutokana na hilo basi sina shaka yoyote mimi kuwa mama. Lakini sina sababu za kuliangaia sana hilo. Sio kama mshale wa saa unavyotembea lakini kama katika nasfi yangu itokee tu” alisema Khloe alipouliza kuhusu kuanzisha familia na mcheza kikapu Thompson.

Hata hivyo Thompson ana mtoto wa kiume wa miezi minane aliyempata na mwanamke mwingine jambo ambalo halionekani kabisa kuwa tatizo kwa Khloe Kardashian.

 

 

Comments

comments

You may also like ...