Header

Lil Wayne adai amejiunga na Roc Nation

Lil Wayne ni kichwa kingine ndani ya label inayozidi kukusanya manguli kwenye hip hop, Roc Nation. Wayne amenukuliwa akisema kuwa amejiunga na label hiyo ya Jay Z.

Akiwa kwenye show katika chuo kikuu cha Slippery Rock huko Pennsylvania, Weezy alisema, “Is it cool if I just say it? It’s the Roc! You know I’m a member of that team now.”

Weezy amekuwa na ukaribu na Hov kwa muda sasa ambapo mwaka 2015 alisaini mkataba wa ushirikiano na Jay Z kupitia Tidal na kuwa wakati aliwahi kujiita R-O-C millionaire.

Kwa miaka mingi Lil Wayne amekuwa akimchukulia Jay Z kama mtu wa kumwangalia katika muziki.

Comments

comments

You may also like ...