Header

‘Mashabiki wabaki na ushabiki wasiingilie maisha yangu’ – Barakah The Prince

Wiki mbili zilizopita kituo cha Dizzim Online kilikuwa na Dizzim Private Party ambayo ilialika wasanii kibao na moja ya mastaa walioalikwa ni Barakah The Prince kutoka Lebo ya Rock Star 4000 ujio ambao Mashabiki wengi wanaooendekeza u’team walimshambulia mitandaoni kwa kumuita majina mbalimbali baada ya kupiga picha na Meneja wa Diamond Platnumz ‘Babu Tale’ .

Baada ya maneno ya Mashabiki kumshambulia Barakah The Prince leo amefunguka kwa mara ya kwanza kuwa yeye kitu ambacho hakipendi ni mashabiki kumuingilia kwenye maisha yake binafsi hususani kwenye maamuzi yake.

Sidhani kama kuna mtu ambae anaweza kunipa limit kukutana na watu ambao sina nao matatizo hususani kwenye masuala ya kibiashara,Mimi niliitwa kwenye Party ya Radio na nilikutana na Tal ujue Tale ni mtu ambae huwa ananishauri vitu kibao!! Tukapiga picha na tale akaiposti baada ya hapo ile picha ndiyo ikaanza kuleta utata heti kwa nini umepiga picha na Tale? kwani Tale ni shetani mpaka nisipige nae picha? Hapo ndiyo ndiyo nikaanza kumaindi kwani hao mashabiki wanajua Backup anayonipa?Wakati hawajui kuwa Tale ni mtu ambae yupo kwenye Industry muda mrefu na huwezi shabiki kunipangia mtu wa kukutana nae“Alisema Barakah The Prince kwenye mahojiano yake na East Africa Radio.

Aliendelea kuwaonya mashabiki kwa kusema “Nawaomba mashabiki wabaki na ushabiki wasiingilie maisha yangu Private kwa sababu hao wanahitaji kuona ngoma kali na video kali ila sio kuingilia maisha yangu binafsi “

 

Comments

comments

You may also like ...