Header

Mrisho Mpoto atoa funzo kwa watanzania

Msanii wa muziki wa Bongo Fleva na mkali wa mashairi Mrisho Mpoto ametumia utashi wake kwa kufikisha ujumbe kwa watanzania kwa kutumia hadithi iliyojaa ujumbe mzito wenye lengo la kuwaweka sawa watanzania.

Mrisho Mpoto alitumia hadithi fupi kufikisha ujumbe kwa Watanzania kwa kuwapa hadithi fupi iliyojaa mafunzo kibao kwa yule atakaejifikirisha,Soma hapa hadithi yake kisha utafakari ujumbe huo kwa kina.

Mwanamke mmoja alikuwa akifanya kazi katika kiwanda cha kusindika nyama. Siku moja baada ya kumaliza kazi zake pale kiwandani alienda katika chumba chenye freezer (cold room) ambako nyama zilikuwa zikihifadhiwa kukagua vitu fulani. kwa bahati mbaya wakati yupo kwenye hicho chumba cha ubaridi mlango ulijifunga na kijilock kwa nje. na hakukuwa na msaada wa kuweza kuufungua mpaka kuwepo mtu wa nje.

Ingawa alilia na kupiga kelele za kuomba msaada wa kufungiliwa lakini kelele hizo hazikuwa rahisi kusikika nje ya hicho chumba kidogo, na wafanyakazi wengi pale kiwandani walikuwa washaondoka.

Masaa matano baadae akiwa katika hali ya kukaribia kukata roho kutokana na baridi kali ya hicho chumba, mlinzi wa geti la kiwanda hicho alifungua mlango wa cold room alimokuwamo yule mwanamke. Na baadae baada ya kutolewa na kupata nafuu alipata wasaa wa kumuuliza yule mlinzi ilikuwaje na akafungua mlango wa cold room wakati ilikuwa si ratiba yake na vile vile si kazi yake?. Maelezo ya yule mlinzi, ”nimefanya kazi kwenye hichi kiwanda kwa miaka 38 sasa, mamia ya wafanyakazi wanatoka na kuingia kiwandani lakini wewe peke yako kati ya wote uliyekuwa ukithubutu kunisalimia asubuhi na kuniaga kila jioni unapoondoka kiwandani, wengine wanani-treat kama mtu nisye na thamani na ambaye sipo katika ulimwengu huu.

Leo ulipokuja kazini asubuhi ulinisalimia kama kawaida ya tabia yako ya kujali ilivyo ”uliniambia habari za asubuhi na tukafurahi kwa dakika mbili, lakini leo baada ya muda wa kazi kuisha sijapata kwa heri yako na ile ya kunitakia joni njema na kubaki salama. Hivyo nilachukua uamuzi wa kuzunguka kwanza humu ndani kuangalia kama upo kwa sababu kujali kwako kumekuwa kukinifanya na mimi nionekane ni mtu katika ulimwengu huu.

Kwa kutokupata farewell yako siku ya leo nikagundua tu kuna baya litakuwa limekupata. na ndipo nilipokukuta kwenye chumba cha barafu.

FUNZO

Ishi vizuru na kila mtu, be humble to every one, mheshimu kila mtu wakubwa na wadogo. Try to have an impact on people who cross your path every day kwa sababu huwezi jua kesho yako imebeba kitu.

Comments

comments

You may also like ...