Header

Neymar kuikosa El Clasico

 Neymar atakosa kwenye mchezo wa El Clasico dhidi ya Real Madrid Aprili 23 hii ni baada ya Mbrazil huyo wa Brazil kukumbana na adhabu ya kufungiwa michezo mitatu ya ligi  kwa utovu wa nidhamu.
Kufungiwa kwa Neymar kunatokana na matukio mawili yasiyo ya kiungwana aliyoyafanya Jumamosi iliyopita kwenye mchezo wa La Liga uliomalizika kwa klabu yake ya Barcelona kufungwa mabao 2-0 na Malaga huko LaRosaled
Katika mchezo huo Neymar alitolewa uwanjani katika dakika ya 60 baada ya kuonyeshwa kadi mbili za njano.Kadi ya kwanza ya njano ilitokana na kuzuia upigwaji wa faulo kwa kwenda kufunga kamba za viatu mbele ya mpira huku kadi ya pili ikitokana na kumchezea madhambi Diego Llorente.Kosa hilo adhabu yake ni kukosa mchezo mmoja.
Lakini wakati anaelekea kwenye vyumba vya kubadilishia nguo,Neymar alifanya utovu mwingine wa nidhamu baada ya kunaswa akimkejeli mwamuzi msaidizi kwa kumpigia makofi tukio ambalo ni kinyume cha taratibu na adhabu yake huwa ni kufungiwa.Ambapo Neymar amefungia michezo miwili zaidi na jumla kuwa amefungiwa michezo mitatu kwa makosa hayo mawili.

Comments

comments

You may also like ...