Header

Stamina aikimbia mitandao ya kijamii, kishindo cha kurudi kitawashangaza

Rapa mmiliki wa bendera ya hip hop ya Morogoro Stamina Shorwebwenzi anayefanya  vizuri na kazi yake ‘Nitampigia’ aliyomshirikisha Mr. Blu ametoa sababu ziliomuweka mbali na mitandao ya kijamii kwa kipindi kisichopungua mizezi miwili.

Akizungumzia ukimya wake kwa muda tangu kuachia kazi yake ya mwisho na Mr. Blu, Stamina amesema kuwa amekuwa chimbo akiandaa album yake ya pili iliyotajwa kuwa na ngoma 17 na kuonekana kuwa miongoni mwa wasanii watakaoshirikishwa katika album hiyo ni muimbaji Maua Sama kwasababu tayari wameshaingia location kushoot kolabo yao ngoma iliyoonekana kuwa itafuata kuachiwa.

“nina miezi miwili  sijapost kitu chochote, sipo instagram, sipo WhatsApp…sipo popote unapopajua wewe, mtandao wowote huwezi kunikuta mimi. Nimakusudi nimefanya, eheee!!…nimekuwa kimya kwasababu kuna vitu navifanya na ni hivi hivi vya muziki so sihitaji interference ya kitu chochote kile…” Alisema Stamina. Mbali na hicho Stamina alisema kwa sasa ameamua kufanya kazi zake chini ya usimamizi imara.

Akizungumzia sababu za kujikabidhi kwenye mikono ya menejimenti Stamina amesema kuwa ili aweze kupiga hatua zaidi katika muziki ni vyema kushirikiana na watu wenye upeo wa biashara ya muziki kama njia ya kugawana majukumu ya kuongeza alichoshindwa kukipata kipindi alichofanya kazi kwa kujitegemea.

“muziki sometimes inabidi uwape watu majukumu, tumefanya hizi kazi wenyewe…ngoma yangu ya kwanza natoa ilikuwa mwaka 2009 unaweza ukaona ni miaka mingapi nimefanya kazi mwenyewe kwahiyo sometimes tunawapa watu majukumu ambao wanaweza kakutoa hapa wakakupeleka pale…kama unavyoona nilikuwa mvivu wa video lakini this time nishashoot video tatu zipo ndani zimekaa” Aliongeza Stamina alipokuwa akiongeza na HZB Tv.

Hata hivyo Stamina amesema kuwa kuna mengi makubwa ambayo yanapangwa kuhusu muziki wake kwakuwa ameingia katika mikono ya menejimenti imara kiabishara na kuongeza kuwa kitakachofuata kitawashangaza mashabiki kakuwa kuna uwezekano wa kupoteza kila kilichopo kwenye akaunti ya Instagram na kuanza ukurasa wa kutengeneza fanbase ya kujiweka karibu na mashabiki mitandaoni upya.

Kuhusu maenejimenti Stamina hakutaka kusema chochote bali alibainisha kuwa ni kampuni ya wahusika wanaofahamika katika kufanya shughuli hizo.

Comments

comments

You may also like ...