Header

Wakazi amshauri jambo Waziri Mwakyembe

Baada ya tamko la Waziri wa habari,Sanaa,Utamaduni na Michezo Dk Harrison Mwakyembe kutoa tamko kwenye mkutano na waandishi wa habari kuwa yupo mbioni kukutana na Diamond Platnumz kwani anaamini ni moja ya Wasanii wanaozingatia masuala ya hati miliki hatimae Rapa wakazi amempa ushauri Mh Mwakyembe.

Wakazi amesema kitendo cha Waziri wa Habari kukutana na msanii mmoja mmoja ni kinyume na matakwa ya Serikali ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania kwa kuandika “Alafu mfumo wa Waziri kukaa na msanii mmoja mmoja umetoka wapi wakati Rais @MagufuliJP alikataza Alisema serikali ita deal na vyombo rasmi”

Kuhusu ishu ya Copyrights Wakazi alianza kwa kumshauri waziri Mwakyembe kwa kumwambia ashirikiane na Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji Mh Charles John Mwijage ili kuweza kulijadili kwa undani.

Wasanii tuna deal na Wizara Tatu: Habari Michezo na Sanaa, Viwanda na Biashara, Tamisemi. Issue za Copyright zipo chini ya Mwijage“ameandika Wakazi kwenye ukurasa wake wa Twitter.

Aliendelea kutoa ushauri kwa kusema “Nadhani Dr Mwakyembe ungem consult Mh Charles Mwijage kwanza. That’s how Mh Nape Nnauye was doing. Tulikuwa tunakaa vikao na both Ministers”

Kuhusu ishu ya kukaa na msanii moja mmoja Wakazi alisema “Kwanini Waziri useme utakaa na Diamond ku discuss “haki miliki” badala ya kukaa na Shirikisho la Muziki na TUMA. Ndio vyama vyetu rasmi,Ila kuhusu haki miliki, Diamond hapana. He doesn’t know it the way Kamati yetu inavyojua, kamati iliyochaguliwa na all artist by the way”

Akitaja majina ya Wasanii ambao wapo kwenye Kamati iliyochaguliwa na Wasanii ni MwanaFA, Lameck Ditto, Khadija Kopa, Ally Choki, Aika, Wakazi, Nikki Wa Pili, VeeMoney, Keisha, Kalapina, Ado Novemba na Babu Tale.

 

 

 

Comments

comments

You may also like ...