Header

Breaking News: Aliyewahi kuhusika kwenye kazi za R Kelly, Britney Spears, Adele afariki Dunia

SONY DSC

Mshindi wa tuzo za Grammy, muandisi na mkongwe wa muziki katika upande wa mastering duniani Tom Coyne amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 62. Mbali na watu mashuhuri kupata taarifa za kufariki kwake mpaka sasa chanzo cha kifo chake hakijafamika.

Kufuatia watu wa karibu maarufu na wasio na umaarufu zilifuliliza jumbe kupitia mitandao ya kijamii za kutuma salamu za rambi rambi huku wakionesha kushindwa kuamini kama wapenzi wa muziki na watayarishaji wenzake hawatamuona tena. Tom Coyne amesifika kwa kufanikisha kazi za wasanii wakubwa duniani kama George Michael, Beyoncé, Ariana Grande, Maroon 5, Tribe Called Quest, Macklemore, Ryan Lewis, One Direction, Ellie Goulding, Destiny’s Child, R Kelly, Britney Spears, Adele, Mark Ronson na kazi nyingine nyingi ikiwemo baadhi ya album kubwa za wasanii wa hip hop za miaka ya 90.

 

Wafuatao ni baadhi ya watu mashuhuri waliotuma salamu za rambi rambi kupitia mitandao ya kijamii hasa Twitter.

 

 

Comments

comments

You may also like ...