Header

Dk Mwakyembe aipongeza TFF

Wakati kikosi cha vijana chini ya umri wa miaka 17 (Serengeti Boys) kikiendelea kujifua na kambi huko mjini Rabat nchini Morocco ambayo imeandaliwa kwa ajili ya fainali za vijana za Afrika zitakazo unguruma mwezi ujao nchini Gabon.

Ofisa habari wa shirikisho la soka nchini TFF Alfred Lucas amesema taarifa walizozipokea kutoka nchini Morocco zinaendelea kuridhisha kuhusu kambi ya vijana wa Serengeti Boys ambayo ilianza rasmi juma lililopita.

Alfred amesema wakati kambi hiyo ikiendelea vyema Serengeti boys ipo katika maandalizi ya mwisho ya kucheza mchezo wa kwanza wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya Gabon.

Kuhusu mpango wa kuichangia timu ya taifa ya vijana ya Serengeti Boys, Alfred amesema zoezi hilo bado linaendelea na amewataka wadau wa michezo nchini kujitahidi kuichangia timu hiyo ambayo imebeba jukumu la kuiwakilisha Tanzania kimataifa kwa mwaka huu 2017

Wakati huo huo waziri wa habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Harrison Mwakyembe ameendelea kulisifia shirikisho la soka nchini TFF kwa mpango wao wa kuiandaa na kuiendeleza timu ya taifa ya vijana (Serengeti Boys) sambamba na timu nyingine za vijana.

Mwakyembe amewapa sifa hizo TFF akiwa bungeni mkoani Dodoma, huku akiwataka viongozi wa vyama vingine vya michezo kuiga mfano wa shirikisho hilo la soka.

Comments

comments

You may also like ...