Header

Hatimae AC Milan yauzwa kwa Wachina

Klabu kongwe ya nchini Italia AC Milan inayomilikiwa na Makamu wa Rais wa Zamani wa Italia Silvio Berlusconi ameuza klabu hiyo kwa kampuni maarufu ya kichina ya Rossoneri Sport Investment Luxembourg.

Silvio Berlusconi alianza kuimiliki klabu ya AC Milan tangia mwaka 1986 ameiuza kwa wawekezaji hao wa kichina kwa kitita cha Euro Milioni (£740) na kuweka wazi kuwa ameingiza faida kubwa kwa mauzo hayo.

AC Milan ambayo haijashinda taji lolote kwa miaka misimu mitano mfululizo tangia mwaka 2011 huenda ikarejea kwenye ushindani kwani ni Timu ya pili kuwa na makombe 7  ya Klabu Bingwa ikiwa nyuma ya Real Madrid yenye makombe 10.

Hata hivyo kampuni hiyo iliyonunua imemuhitaji Berlusconi kufanya nae kazi kama Rais wa Klabu hiyo lakini ameitolea nje kampuni hiyo.

Comments

comments

You may also like ...