Header

Mihadarati,kiburi vyamponza Tory Lanez

Msanii na Rapa kutoka Canada Tony Lanez amejikuta mikononi mwa polisi huko Florida nchini Marekani baada ya kukutwa na silaha na misokoto kadhaa ya mihadarati kinyume na sheria.

Taarifa kutoka kwenye mtandao wa XXL zinadai kuwa Lanez alikuwa na Silaha kwenye Ndinga yake na Misokoto 20 ya Bangi,Pia mkali huyo wa ‘LOVE’ alikutwa akiendesha Gari bila Leseni na kuwatolea maneno machafu maaskari waliokuwa wakimhoji .

Hata hivyo mapema jioni ya leo mtandao wa TMZ umeripoti kuwa Rapa huyo ameachiwa na Polisi baada ya kulipa faini ya kitita cha Dola 1,000 na kupewa onyo kali kwa rapa huyo.

 

Comments

comments

You may also like ...