Header

Ross Barkley aitaitamani michuano ya Klabu Bingwa Ulaya

Kocha mkuu wa  Everton Ronald Koeman ameweka wazi kitu ambacho kinamfanya kiungo wao mshambuliaji Ross Barkley  asisaini mkataba mpya na klabu hiyo.

Akizungumza na Sky Sport amesema kuwa kitu ambacho kinamfanya Ross asisaini mkataba na timu hiyo kuwa anaitaji kucheza michuano ya Klabu Bingwa Barani ulaya  msimu ujao kitu ambacho Everton kwao ni kigumu kutokana nafasi yao kwenye ligi.

“Nikweli nimefanya mazungumzo na Ross juu yakubaki klabuni ila ameniambiwa anataka kucheza Michuano ya Klabu Bingwa hicho ndio kigezo chake cha kwanza ili asalie klabuni” Alisema Koeman

Barkley mwenye umri wa miaka 23 anatajwa kuwa ya viungo bora sana kunako ligi kuu nchini Uingereza kutokana na kipaji chake na uwezo wake mkubwa Uwanjani.

 

Comments

comments

You may also like ...