Header

Abdi Banda kutimkia South Africa

Beki wa kati wa Simba Abdi Banda baada kusimamishwa kucheza ligi kuu Tanzania Bara Kwa kosa la kumpiga ngumi kiungo wa Kagera sugar George Kavilla wakati akiwa hana Mpira.

Taarifa kutoka ndani ya Klabu ya Simba zinasema kuwa Banda anaelekea South Afrika kufanya majaribio kwenye timu moja huko.

Akizungumzia swala hilo Abdi amesema kuwa”Ndio naenda Afrika kusini Kwenye Mazungumzo na timu moja huko na sitakaa muda mrefu maana naenda kwa Mazungumzo kuhusu mkataba na si kufanya Majaribio Sizani kama hata wiki itaisha”

Mkataba wa Banda na Simba unaisha mwisho wa msimu Banda yuko huru kufanya mazungumzo na timu yoyote lakini Simba walimpa mkataba mpya ili ausome na akikubaliana nao ausaini lakini wakala wa Bandaa alisitisha kusaini mkataba mpya mpaka mwisho wa msimu.

Comments

comments

You may also like ...