Header

BreakingNews: Uwanja wa CCM Kirumba kutumiwa kwa Mechi za Kimataifa

Baada ya muda mrefu shirikisho la soka Nchini Tanzania TFF limekuwa likituma  maombi ya uwanja wa CCM Kirumba wa jijini mwanza kutumiwa kwa michuano ya mechi za Kimataifa hatimae Ombi hilo limekubaliwa.

Akithibitisha Taarifa hizo Rais wa TFF Jamal Malinzi kupitia ukurasa wake rasmi wa Twitter ameandika “Wana Mwanza hongereni uwanja wa CCM Kirumba umepitishwa na CAF&FIFA kutumiwa kwa mechi za Kimataifa”

Mwanzoni mwa mwezi uliopita klabu ya Yanga ilituma Ombi la kuutumia uwanja huo kwenye mchezo wao dhidi ya MC Alger lakini Ombi lao liligonga mwamba kwani uwanja huo ulikuwa bado haujakidhi vigezo

Comments

comments

You may also like ...