Header

G-Nako awashangaa wasanii wenye uoga wa kuachia nyimbo

Msanii kutoka katika kampuni ya ‘Weusi’ G Nako aliyejizolea sifa kibao kwa uwezo wake wa kufanya viitikio vya kufanya ngoma iwe kubwa ashangazwa na uoga wa baadhi ya wasanii wanaogopa kuachia nyimbo kindi ambacho masuala ya kisiasa kuonekana kuchukua nguvu zaidi.

Akizaungumzia kinachosemekana kuwepo kwa wasanii baadhi walioshindwa kuachia nyimbo kipindi hiki kwa sababu za kusema kuwa siasa imefunika muziki ni jambo linalomshangaza sana na kusema kuwa hakuna chochote kinaweza kuzuia nguvu ya muziki kwakuwa haya mambo yanayotokea ni ya muda tu na muziki ni hisia yenye uwezo wa kuishi kwa muda mrefu.

“mimi nashangaa wasanii wanaoogopa kutoa nyimbo na vitu kama hivyo, hakuna chochote kinawetuzuia sisi kwasababu muziki unasimama kama muziki…muziki ni hisia. Huwezi kuniambia kwamba kuna group la watu wa aina fulani sasa hivi ukilipigia muziki mzuri haliwezi kuelewa kwasbabu kuna vitu fulani vinaendelea” Alisema G Nako alipokuwa akihojiwa na Ladhaa 3600 ya E Fm na Jabir Saleh.

Hata hivyo G amesema kuwa kabla ya wazo la kuachia wimbo wao wa pamoja na Joh Makini na Nikki wa Pili wa ‘Madaraka ya kulevya’ walikuwa na mpango wa kuachia goma nyingine tofauti bila kujali hali ya chochote kinachoendelea, bila kujali kina nguvu gani na wanaamini kwa ubora wa hiyo kazi ingefanya vizuri bado, na ameongeza kuwa mwaka huu wana mpango wa kuachia nyimbo nyingi tofauti na miaka iliyopita.

Comments

comments

You may also like ...