Header

Mchekeshaji wa Churchil Show ya Kenya afariki

Mchekeshaji maarufu kupitia kipindi cha runinga cha uchekeshaji cha Churchill (Churchill Show)  ‘Emmanuel Makori Nyambane’ a.k.a ‘Ayeiya Poa Poa’ amefariki dunia katika ajali ya gari iliyotokea usiku wa jana.

‘Ayeiya Poa Poa’ alifariki pale pale mara baada ya gari alilokuwa kuugonga mlingoti wa nyaya za umeme karibu kabisa na chuo cha ‘Catholic University of Eastern Africa (CUEA)’. Ken Waudo kutoka katika kitengo cha kufanikisha kipindi cha ‘Churchill’ kiitwacho Laugh Industry amethibitisha kifo cha machekeshaji huyo.

Hata hivyo ‘Ayeiya Poa Poa’ katika ajali hiyo alikuwa na mkewe, muigizaji wa filamu ya Nairobi Half life ‘Maina Olwenya’, mchekeshaji mwenzake Paul wa Kimani na marafiki wengine. Paul wa Kimani, Maina Olwenya na mke wa Ayeyaa wako hospitalini kwa matibabu.

Comments

comments

You may also like ...