Header

Ray ‘Vicent Kigosi’ achukizwa na kamati ya Saa 72

Muigizaji wa Filamu nchini Tanzania Ray Kigosi amechukizwa na kitendo cha TFF kuweka kamati ya saa 72 ambayo kiukweli amedai imekuwa inaharibu sana mpira wetu wa Tanzania kwani kumekuwa na Figisu figisu.

Ray amesema hayo baada ya jana kamati hiyo kutoa pointi 3 na Magoli matatu kwa klabu ya Simba baada ya Rufaa yao dhidi ya Kagera Sugar ya kumtumia mchezaji wao Mohammed Fakhi aliyekuwa na kadi tatu za Manjano kwenye mchezo ambao Simba walilala kwa goli 2-1.

Mkongwe huyo wa Filamu amesema ni heri ashabikie mchezo wa Mdako kwani Mpira wa miguu ni michosho tuu,Kupitia ukurasa wake wa Instagram kwa kuandika “Mpira Wa Tanzania Daaah….Mpaka Tunatia Huruma Yani Kuendelea Kwa Mpira We2 Labda Kizazi Kipya Kije Sio Hiki Cha Masaa 72″

Hata hivyo hakuishia hapo akamaliza kwa kumshauri swahiba wake JB kuachana na mpira wa Miguu na kuanza kushabikia mdako “JB Bora upende mdako Kuliko Mpira Wa Tanzania Ushuzi Mtupu

 

Comments

comments

You may also like ...