Header

Thibaut Courtois “Hatujaridhika kwa kuwa tuko kileleni”

LONDON, ENGLAND - DECEMBER 31: Thibaut Courtois of Chelsea during the Premier League match between Chelsea and Stoke City at Stamford Bridge on December 31, 2016 in London, England. (Photo by Catherine Ivill - AMA/Getty Images)

Mlinda mlango wa Chelsea Thibaut Courtois amedai kuwa yeye na wachezaji wenzake hawawezi kuridhika kukaa kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu.

Miamba hiyo ya Darajani wamekuwa vinara kwa muda wa miezi mitano, lakini waliangukia pua kwa kipigo cha 2-1 dhidi ya Crystal Palace mwanzo wa Aprili, na Tottenham wamejidhatiti kutumia nafasi zote ambazo Chelsea itateleza tena.

“Kushinda ubingwa, ni sharti tufanye kama ilivyokuwa miezi iliyopita. Ni lazima tujitahidi kushinda mechi kuwa watulivu kwa kila kinachotokea,” Alisema hayo Courtois alipokuwa akizungumza na gazeti la  London Evening Standard

Kikosi hicho cha Antonio Conte kwa sasa kipo kileleni kwa pointi  7 mechi 7 zikiwa zimebakia huku The Blues watakuwa na kibarua kigumu Jumapili watakapoikabiliana Manchester United ya Jose Mourinho katika uwanja wa Old Trafford

Comments

comments

You may also like ...