Header

Willy Paul atetea tabia zake kwa wanaomsema vibaya

Msanii wa muziki wa ijili kutoka nchini Kenya anayefanya vizuri na wimbo wake ‘I do’ aliomshirikisha msanii Alaine Laughton ‘Alaine’ kutoka Jamaica atoa sababu ya mambo yote anayofanya katika maisha yake ya umaarufu na kinachoonekana kama hakustahili kufanywa kutokana uelewa wa misingi ya maisha ya uokovu na muziki wa ijili kwa ujumla.

Akizungumzia mikiki mikkii ya skendo tofauti zinazo mkabili za kubadili akinadada, na tuhuma za kutoelewana na baadhi ya wasanii wenzake Willy Paul amesme akuwa mashabiki na watu wote wanafaa kumuelewa kwakuwa umri wake na usasa wa mambo vinamruhusu kufanya anachokifanya.

“Siwezi kujizeesha wakati umri huo bado sina. Ndio maana nafanya mambo ya umri wangu kama vijana wengine kwa sababu nikivilenga, huenda nikaja kumsumbua mke wangu  nitakapokuwa na familia, jambo ambalo sidhani litakuwa zuri,” Alisema Willy Paul.

Hata hivyo moja ya habari kubwa kuhusu Willy Paul inayoendana na hayo yanayosemwa kuelekwa kwake kutoka kwa mashabiki baada ya safari ya media tour nchini Tanzania alihusishwa na kilichosemwa kuwa alionyesha kumtamani kimapenzi binti mrembo maarufu kama Dj Sinyorita na baada ya kumiminia sifa za uremno wake kuwa anahisi kama imepangwa kwake kuoa nchini Tanzania kutokana na urembo wa Dj huyo.

 

Chanzo: Swahili Hub.

Comments

comments

You may also like ...