Header

Kagera Sugar watua TFF kupinga pointi tatu za Simba

Klabu ya soka ya Kagera Sugar imeiandikia barua Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) kupinga vikali maamuzi yaliyotolewa na kamati ya saa 72 kwa kuipatia timu ya Simba SC alama tatu.

Kagera Sugar ilidaiwa kumchezesha mchezaji wao Mohammed Fakhi aliyekuwa na kadi tatu za njano wakati walipokuwa wanacheza katika uwanja wa Kaitaba Mkoani Kagera wiki mbili zilizopita.

Barua hiyo imeandikwa na Katibu Mkuu wa klabu hiyo, Hamis Mdaki ambapo ameiomba TFF ifanye marejeo ya maamuzi ya rufaa iliyokatwa na Simba dhidi yao ili haki iweze kutendeka.

                                       Barua ya Kagera Sugar kwa TFF

Hata hivyo Klabu hiyo imewatahadharisha TFF kuwa makini na maamuzi ambayo yanatolewa kwa kuwa watu wengine wana lengo la kuchafua  taswira na heshima ya mpira wa miguu iliyojengwa nchini.

Comments

comments

You may also like ...