Header

Mzee Wenger apoteza matumaini ya Big Four

Kocha mkuu wa Arsenal Mzee Arsene Wenger amekiri kwamba siku hizi chache hazijawa za furaha kwake kufuatia kipigo alichopokea dhidi ya Crystal Palace kwa kichapo cha 3-0

Matokeo hayo yamefanya tumaini la Arsenal kumaliza nafasi 4 za kwanza kuanza kufifia kwani kwa sasa wanashika nafasi ya 6 katika msimamo, pengo la pointi saba kuipata nafasi ya kucheza Ligi ya Mabingwa zikiwa zimebaki mechi nane tu.

Alipoulizwa anaonaje hali ya kikosi chake siku hizi ambazo Arsenal imekuwa vibaya kwenye mkutano wa waandishi  jana Ijumaa, Wenger alijibu: “Si za kufurahisha, kama mnavyofahamu. Nyakati mbaya ni sehemu ya kazi. Tunaelekeza akili zetu kwenye maandalizi na kuhakikisha tunarudi kwenye njia za ushindi.

Arsenal watajitahidi kuweka mambo sawa watakapoikabili Middlesbrought Jumatatu ya Pasaka.

Comments

comments

You may also like ...