Header

Penzi la Jux na Vanessa Mdee bado kitendawili 

Baada ya kuenea tetesi kuwa mastaa wawili wa Bongo Fleva Mix na Vanessa Mdee kuwa wamemwagana bado taarifa hizo zinakosa majibu kwani kila mmoja anatoa majibu ya mafumbo.

Jana Jux alikuwa ni moja ya Wasanii walioalikwa kwenye kipindi cha FNL cha EATV na moja ya maswali aliyoulizwa ni kuhusu tetesi za yeye kumwagana na Mpenzi wake Vanessa Mdee.
Jux alisema yeye hana Taarifa yoyote kuhusu kuachana na Vanessa na ndiyo mara yake ya Kwanza kusikia hicho kitu.

“Mimi sijui chochote kuhusu hizo tetesi ndiyo wewe unaniambia mbona tuko poa hatuna tatizo”Alisema Jux

Alipoulizwa kuwa kwa sasa yupo single au yupo na Vanessa kwenye mahusiano alisema “Mimi sio single boy nipo na Mtu na tunapendana nae ”

Alipoulizwa ni Vanessa au ni mrembo mwingine alijibu “Kuhusu ni nani natoka nae non of your business”

Jux na Vanessa kwa muda mrefu wamekuwa mbali kila mtu na mishe zake tofauti na kipindi cha nyuma ambapo walionekana kuwa karibu hata kwenye mitandao ya kijamii.

Comments

comments

You may also like ...