Header

RC Makonda akoleza vita dhidi ya maharamia wa kazi za wasanii mbele ya JPM

Mkuu wa mkoa wa jiji la Dar es salaam Mheshimiwa Paul Makonda amewasilisha matatizo yanayoikumba bongo movie na ni jinsi gani anayafanyia kazi kwa faida ya wanatasnia na watanzania kwa ujumla jambo lilowasilishwa mapema katika uzinduzi wa mabweni mapya ya chuo kikuu cha Dar es salaam (UDSM) ambapo mgeni rasmi alikuwa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli.

Akiwasilisha mambo hayo muhimu kwa niaba ya wasanii wa bongo movie mbele pia ya baadhi ya wasanii maarufu waliofika katika uzinduzi huo, Paul Makonda amesema kuwa atahakikisha hakuna kilio tena kitakachosikika pia itawekwa miundo mbinu itakayomjengea mzingira kila msanii kupata haki ya kazi zake.

 

 

Comments

comments

You may also like ...