Header

Haji Manara atupa jiwe gizani kwa Wanajangwani

Pamoja na Simba kupata sare ya bila kufungana dhidi ya Toto Africans, Msemaji wa Simba Haji Manara anaamini bado Simba ina nafasi ya kubeba ubingwa kwa kuwa iko kileleni kwa tofauti ya pointi sita

Manara amesema hayo kupitia akaunti yake ya Instagram kuwa anawapongeza Toto kwa kuapata sare dhidi ya mabingwa watarajiwa na wako juu kwa alama sita sasa.

Aliyenacho mkononi ni tofauti na anayesubiri kupata. Tuko kileleni kwa tofauti ya pointi sita, tusubiri kinachokuja. Ila niwaambie, nguvu za ubingwa ziko palepale na ongereni toto kwa kupata sare na mabingwa watarajiwa“Aliandika Manara

Simba imefikisha pointi 62 na Yanga inafuatia ikiwa na pointi 56, hata hivyo Simba imecheza mechi 27 na Yanga ina pungufu miwili kwa kucheza 25.

Comments

comments

You may also like ...