Header

Kuhusu mapenzi yao na Vanessa, Jux aelezea hali halisi

Msanii wa bongo fleva na mmiliki wa brandy ya ‘African Boy’ Juma Jux ameweka sawa taarifa zilizo sambaa sana kuhusu kuchana na mpenzi wake ambaye pia ni msanii mwenzake Vanessa Mdee.

Akiwajibu wanaozusha kuhusu wawili hao kuachana Jux amesema kuwa sio habari za kweli kwamba kwasasa yuko single na alipoulizwa kama bado wako kimapenzi na Vanessa alijibu “kwanza kabisa hiyo habari sio ya ukweli na kama sio ya kweli inamaana ukweli ninao mimi…that is my business…i don’t wanna talk about that” innagwa alisema kuwa mbali habari habari za kuwa hawako pamoja lakini watu wanafaa kujua kuwa yuko katika mahusiano.

Hata hivyo Jux amehaidi baada ya ngoma mbili za mwisho alizoachia mwishoni mwa mwaka jana ‘Wivu’ na ‘Juu’, mwaka huu  atakuja na ujio mwingine mkubwa wenye audio kali na video yenye ubora na nzuri soon “natoa nyimbo mimi kama Jux soon”. Pia Jux amewataka mashabiki wa Vanessa wakae mkao wa kula kupokea kolabo kubwa kubwa ambazo tayari zimeshakamilika na album ya ‘Money Mondays’ inayotegemewa kutoka karibuni.

 

Chanzo: EA TV.

Comments

comments

You may also like ...