Header

Tekno Miles amwaga mchele kwenye kuku wengi

Msanii na mtayarishaji wa muziki kutoka Nigeria anayefanya poa na ngoma ‘Yawa’ yenye muda wa wiki tatu tangu video rasmi ya wimbo itoke Tekno, ni wiki sasa tangu kutibitisha kuwa katika mahusiano ya kimapenzi msanii mwenzake Lola Rae baada ya ficho la penzi lao hilo kwa muda.

Mwimbaji Lola Rae

Wakiwa katika moja kuwanja cha starehe Lola Rae na Tekno walionekana katika busu zito la mahaba tukio lililoonyesha kuwa kwa muda walishindwa kujizui kiasi cha waliokuwa karibu nao waliweza kuchukua video za tukio hilo la mahaba yao.

Msanii huyo wa kike Lola Rae ni mzaliwa wa mwaka 1991 na mwenye asili ya Ghana na Uingereza kutoka kwa baba yake na amepata umaarufu zaidi kupitia muziki mwaka 2012 kupitia ngoma yake ‘WATCH MY TING GO’ na mwishoni mwa mwaka jana ameachia kazi yake ianyokwenda kwa jina ‘BIKO’ aliyomshirikisha Davido.

Comments

comments

You may also like ...