Header

Jackson Mayanja awaponda Toto Africans

KOCHA msaidizi wa Wekundu wa Msimbazi Simba Mganda Jackson Mayanja, amesimulia kilichotokea katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Toto Africans uliochezwa juzi kwenye Uwanja wa CCM Kirumba.

Mayanja amesema Toto Africans waliharibu mipango yao ya kuondoka na pointi tisa Kanda ya Ziwa, kutokana na mbinu walizotumia za kuchelewesha dakika katika mchezo huo.

Mchezo ulikuwa mzuri, Toto Africans wamecheza mpira wa kuchelewesha muda wametunyima pointi tatu, malengo yetu yalikuwa pointi tisa Kanda ya Ziwa, tumeondoka na pointi saba tu,” Mayanja aliliambia gazeti la Bingwa

Katika mchezo huo, Simba walishindwa kuondoka na pointi zote tatu ili waweze kujiweka katika mazingira bora ya kutwaa ubingwa msimu huu, baada ya kutoka sare tasa na wenyeji hao wa Jiji la Mwanza.

Comments

comments

You may also like ...