Header

Jacob Steven “JB” awapa somo Simba Sports Club

Msanii kutoka kiwanda cha Bongo Movie Jocob Steven  ameiasa klabu yake pendwa Simba Sports kutochukua wachezaji mizigo na klabu nyingine kuacha kuchukua wachezaji wasio na tija kwa timu zao kuja kucheza Ligi Kuu Tanzania Bara.

JB alitoa ushauri huo wakati akionge na mtandao wa Simba Sports Club na kusema kitendo cha klabu kusajili wachezaji kutoka nje ya nchi ambao uwezo wao ni mdogo kwanza inawatia hasara klabu kwa kumlipa mchezaji huyo wakati hakuna jambo analofanya kusaidia klabu zaidi ya kuishia kukaa benchi.

Ushauri wangu mimi kwa ‘technical’ benchi ni kwenye hao ma wachezaji professional ambao tuna wachukua kutoka nje ya nchi, unajua ni hasara sana mtu  ambaye amechukuliwa kutoka nje kama professional analipwa pesa nyingi kuliko wenzake akawa nje ya mchezo. Lazima tuwe na uhakika na wachezaji tunao wachukua kutoka nje ya nchi na lazima wawe na uhakika wa kucheza kwenye ‘First eleven’ kinyume na hapo tutakuwa hatuzitendei haki pesa zetu, wakati mwingine siwalaumu sana maana kuna mchezaji unaweza kumuona mzuri akija huku asifanye vizuri sana” alisema Jb

 

Muigizaji huyo alienda mbali na kuzidi kusikitiza kuwa watu wanaochukua wachezaji hao kutoka nje lazima wajihakikishie kuwa mchezaji anayetoka nje kuja nyumbani lazima awe na uwezo mkubwa kuliko wachezaji wetu wa ndani ili kuwajengea wachezaji wetu viwango bora.

Comments

comments

You may also like ...