Header

Jose Mourinho afuraia kuiangamiza Chelsea

Meneja wa Mashetani wekundu Mreno mwenye maneno mengi Jose Mourinho emeeleza furaha yake baada ya kuifunga Chelsea Jumapili, lakini amesisitiza ni kwa sababu tu ni vinara wa sasa wa Ligi Kuu nchini Uingereza

Chelsea hawakuwa na ubishi zaidi ya kupokea cha 2-0 Old Trafford, Marcus Rashford na Ander Herrera wakiwapa Manchester magoli na kuanza kuvuruga mbio za Chelsea kwenye ubingwa.

Sina furaha nyigine zaidi ya kuifunga Chelsea tumewafunga vinara. Haijalishi kama kinara wa msimamo wa ligi ni Chelsea au ni timu nyingine, lakini tumewafunga bila utata. Hakuna yeyote anayeweza kutilia shaka ushindi wetu.”Mourinho Aliambia BBC Sports

Matokeo hayo yameiwezesha Man United kupanda hadi nafasi ya tano kwenye msimamo wa ligi, pointi nne nyuma ya Man City, wakati Chelsea sasa ikiizidi pointi nne tu Tottenham Hotspur

Comments

comments

You may also like ...