Header

Kala Jeremiah awachana marapa wa Bongo

Rapa kutoka Tanzania Kala Jeremiah amefunguka kwa kile anachoona kuwa Marapa wengi wa siku hizi wanakiuka miiko ya ya hip hop kwani nyimbo nyingi zinakosa uhalisia kitu ambacho kinapelekea kupoteza ladha.

Kala amesema tangia zamani muziki wa hip hop ulikuwa unapendwa kwa ujumbe wake wa uhalisia wa maisha tofauti na siku hizi ambapo wasanii wengi wanatunga mistari ya kusifia vitu walivyonavyo.

Kwangu mimi naamini hip hop ni kitu kinachotakiwa kije na ujumbe,kije na kitu fulani ndani yake na actually ilikuwa hivyo zamani hapa Bongo,yaani wimbo unakuta una ujumbe mzuri ambao unalenga jambo moja kwa kulichambua kwa kina yaani hadi msikilizaji anapata hamu ya kushawishika kurudia na kurudia HIP HOP ni uhalisia “Amesema Kala Jeremiah kwenye mahojiano yake na East Africa Radio.

Kala Jeremiah ameendelea kuwachana wasanii wa Hip Hop kuwa Uhalisia ni moja ya nguzo muhimu kwenye muziki huo hivyo kama ni biashara itakuja baada ya kufanya kazi nzuri “Ombi langu tu kwa wasanii wa muziki wote tukumbuke kuwa kuna uhalisia wa Hip hop pia,tufanye vitu vyetu vyote lakini waangalie kuwa tupo kwenye mstari gani mimi naamini hip hop nzuri yenye ujumbe mzuri itageuka tuu kuw biashara

Comments

comments

You may also like ...