Header

Kenya kuhalalisha matumizi ya Bangi

Kenya ipo mbioni kuhalalisha matumizi ya Bangi hii ni kutoka na zaidi ya Wakenya 1,400 wanaunga mkono ombi la kutaka kuidhinishwa kwa matumizi ya mmea huo baada kuwasilisha hoja hiyo mbele ya bunge la seneti.

Ombi hilo la mtafiti Gwada Ogot litaidhinishwa haitakuwa haramu kupanda ama hata kuuza bangi nchini Kenya,Ogot anasema kwamba matumizi ya kiafya pamoja na utumizi wa mmea huo viwandani unaojulikana kwa jina la sayansi kama Cannabis sativa una faida nyingi.

Akielezea faida za mmea huo amesema kuwa matumizi ya mmea huo yataimarisha hali ya uchumi,ingawaje Sheria za Kenya zinapiga marufuku matumizi ya bangi na kwamba mtu yeyote atakayepatikana akitumia dawa hiyo atashtakiwa kwa uhalifu.

                                                                      Chanzo : Mtandao wa BBC

Comments

comments

You may also like ...