Header

Lulu afunguka sababu za kusherehekea kimya kimya Birthday yake

Jana ilikuwa ni siku ya kuzaliwa kwa Msanii wa Bongo Movie Elizabeth Michael ‘Lulu’ na jambo la kushangaza kwa mrembo huyo ni kwamba hakuposti kabisa kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii kitu ambacho kiliibua maswali lukuki kwani kwa mastaa wa kike ni jambo gumu sana kutokea.

DizzimOnline ilimtafuta Lulu kuzungumzia ishu hiyo na kusema kuwa ni mabadiliko tu kutokana na umri na pia haoni umuhimu wa kuposti kwani sherehe ya kuzaliwa atasherehekea na watu wake na sio kitu kikubwa kwake.

Mimi nafanya changes kila siku kwenye maisha yangu kwahiyo itafika wakati sioni kama ni kitu kikubwa kwani naongeza mwaka tuu,namshukuru Mungu najiona nakua na siku kama za leo natumia kukaa karibu na familia yangu“Aliendelea kuongea kwa kugusia kwanini hakuposti Instagram.

Kwa sasa hivi watu wanachukulia Instagram au mitandao ya kijamii kama ndiyo kila kitu najaribu kufanya maisha yangu yawe out na social Networks“Amesema Lulu.

Lulu ametimiza miaka 22 tangia kuzaliwa kwake.

 

 

Comments

comments

You may also like ...