Header

Yanga yatoa taarifa kamili ya kikosi kilichokwama Uarabuni

Wachezaji 12 wa Yanga akiwemo Katibu Mkuu wao Charles Boniface Mkwasa, wanaelezwa kuachwa na ndege mjini Algiers nchini Algeria na hii inatokana na wao kushindwa kuendana na ratiba ya shirika la ndege la Turkish Airline.
Klabu ya Yanga kupitia mitandao yake ya kijamii imeeleza kuwa wachezaji wake walichelewa kuendana na ratiba kutokana na foleni za jiji la Algiers hivyo kuachwa na ndege na sio kama taarifa za uzushi zinazozagaa mitandaoni.
Baadhi ya wachezaji wa Yanga SC waachwa na ndege Algeria International Airport baada ya kuchelewa kufika kutokana na jam ya jiji la Algiers. Wachezaji walioachwa na ndege ya shirika la Emirates ni kundi la kwanza . Utaratibu umekwishafanyika kwa kupatia usafiri kwenye ndege nyingine ya shirika hilo kwa ajili ya kuondoka kesho au keshokutwa kulingana na ratiba . Kilichowafanya kuchelewa ni uzembe wa wenyeji wao kuwatafutia polisi wa usalama barabarani kwa ajili ya road clearance. Taarifa hii ni tofauti na habari zinazoenezwa mitandaoni kwamba msafara huo chini ya katibu mkuu umefanya uzembe binafsi kuchelewa ratiba ya ndege “Imeandika Klabu ya Yanga kupitia mitandao ya Kijamii.
Kutokana na hali hiyo wachezaji hao watabaki nchini humo hadi Jumatano hata hivyo bado kuna juhudi  za kufanya waondoke mapema zaidi ili kuwahi nyumbani kwa maandalizi ya mechi za ligi kuu zilizosalia.
Yanga walikuwa nchini humo kucheza mechi ya Kombe la Shirikisho dhidi ya MC Alger na walitandikwa mabao 4-0,Kabla wachezaji wa Yanga walienda Aligeria kwa makundi wengine wakipitia Dubai na wengine Istanbul nchini Uturuki.

Comments

comments

You may also like ...