Header

Gonzalo Higuain aihofia Barcelona

Mshambuliaji wa Juventus Gonzalo Higuain amesema kuwa Barcelona wanaweza kufanya miujiza tena kama yale ya PSG  kuelekea mechi ya marudiano Ligi ya mabingwa.

Bianconeri walishinda 3-0 katika jiji la Turin mechi ya kwanza hatua ya robo fainali, lakini miamba hao wa Catalan walipindua matokeo na kulipa deni la magoli 4-0 dhidi ya Paris Saint-Germain.

Sijui kama ushindi wetu wa mabao 3-0 utatosha, Hatuna budi kupigana Camp Nou kama tulivyofanya Turin. Barcelona walionyesha dhidi ya PSG kwamba wanaweza kufanya miujiza, kadhalika kwetu inawezekana pia ” Higuain alitoa tahadhari, katika mjadala wa mechi hiyo na JTV.

Juve wapo kileleni kwa tofauti ya pointi nane kwenye msimamo wa Ligi kuu nchini Itary ikiwa mechi sita zikiwa zimebaki kumaliza msimu, lakini Higuain haamini kama mbio za Scudetto zimekwisha.

Comments

comments

You may also like ...