Header

John Terry atangaza kuachana na Soka

Baada ya kuitumikia Chelsea kwa muda mrefu Nahodha wa timu hiyo Muingereza John Terry ametangaza kuachana na Soka pale tu msimu huu utakapomalizika tu.

John Terry maeitumikia Chelsea kwa miaka 22  nakufanikiwa kushinda mataji mbali mbali ndani ya klabu hiyo akiwa kama mchezaji wa kawaida tu na kiongozi ambaye mwenye heshima sana hapo Darajani.

Terry ameshinda makombe mbali mbali likiwemo Kombe la Ligi Kuu nchini Uingereza na Klabu bingwa mwaka 2012 huku John akiikosa fainali hiyo ambayo Chelsea ilitwaa Ubingwa kwa kuifunga Bayer Munich kwa changamoto ya mikwaju ya penati.

Nahodha huyu amecheza michezo 713 akifunga magoli 66 na kuchukua jumla ya ndoo za ubingwa 14 na mpaka sasa anashikilia rekodi ya kuwa beki mwenye magoli mengi ndani ya EPL.

Comments

comments

You may also like ...