Header

Muuaji wa Facebook ajiua

Mtu mmoja aliyekuwa anawindwa na polisi huko Pennsylvania nchi marekani aliye tambulika kwa jina la Steve Stephens apona makali ya sheria kwa kosa la kumuua raia mwema katika hadhara ya mtandao.

Siku chache zilizopita serikali ya Marekani ilitoa donge nono kwa mtu atakae weza kumuona na kutoa taarifa kwa vituo karibu cha polisi muuaji huyo aliye ripotiwa kumua mzee mmoja hasiye na hatia kwa kumpiga risasi tukio lililoneshwa moja kwa moja kupitia mtandao wa facebook.

Mzee huyo aliyepigwa risasi alitambulika kwa jina Robert Godwin mwenye umri wa miaka 74 na muuaji huyo baada ya kutekeleza mauaji alianza kutuma ujumbe wa video akijitamba na kuonekana kutojuta kuhusu kitendo cha kikatili alichofanya.

Hata hivyo muda mfupi baadae baada tukio lile liliolaaniwa na wengi vyombo vya usalama vilitangaza dau la dola 50,000 kwa atakayefanikisha kuisaidia polisi kumkamata muuaji huyo aliye pewa jina la”Facebook killer” ambaye taarifa zinasema kuwa kuwa amejiua kukwepa makali ya sheria yaliyokuwa yakihitaji kumfanyia kazi.

Comments

comments

You may also like ...